Fataki ni kampeni ya kuwakinga watoto wa kike na wanawake dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi toka kwa wanaume wanaowalaghai kwa fedha na vitu vya thamani ili kuwapata kimapenzi.
Fataki ni husika ya kufikirika aliyovikwa mwanaume mtu mzima ambaye anarubuni watoto wa kike pamoja na wanawake wengine ili kufanya nae ngono.
Fataki ni baba mtu mzima ambaye anatumia uwezo wake wa kiuchumi/kifedha kuwarubuni watu wa jinsia ya kike kutimiza lengo lake, kutokana na sifa yake hii anafikia hatua ya kubandikwa majina mengine kama ATM.
washiriki wa warsha wamechangia mawazo yao juu ya mambo muhimu ya kuzingatia katika suala zima la mawasiliano kwenye mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.
Washiriki hawa walianisha mambo mawili muhimu, moja likiwa ni suala la upashanaji wa habari ukizingatia tofauti za kijinsia na umri wa jamii lengwa
Jambo la pili liliowekwa bayana lilikuwa ni changamoto katika kushawishi walengwa kwenda kupima virusi vya ukimwi kwa hiari.
Washiriki walijikita katika kutengeneza mawazo na ujumbe madhubuti yanayozingatia mambo haya mawili. Baada ya kutengeneza mawazo haya walihakikisha kuwa yanafanyiwa majaribio. Majaribio haya yalifanywa mara tatu na mara zote hizi tatu walihakikisha kuwa wanayaboresha mawazo yao kutokana na maoni ya wale ambao walifanyiwa majaribio.
Washiriki waliohusishwa na mawazo na majaribio haya walikuwa ni wasanii waigizaji, watayarishaji wa vipindi vya radio, waandishi wa michezo ya kuigiza, pamoja na wachoraji wa viponzo. Kila mmoja alipewa nafasi ya kuweka mchango wake
Mwisho wa warsha washiriki walifanikiwa kutoka na matangazo manne ya radio na viponzo viwili. Matangazo haya yalifanyiwa tena majaribio kwa wasikilizaji na wasomaji na hatimae kufanyiwa marekebisho kutokana na maoni katika mwezi wa September, 2008
No comments:
Post a Comment