Simba, Nyati, Faru, Chatu....haya ndiyo majina ya wanyama yanayoweza kukujia akilini pindi ukiulizwa MNYAMA YUPI NI HATARI ZAIDI KWA MWANADAMU. Well, amini usiamini, kiumbe hatari zaidi ni mdogo mara elfu kadhaa akilinganishwa kiumbo na hao majabali tunaowafahamu. Na udogo wake si katika umbile pekee bali pia hata sauti yake ni ndogo kulinganisha na mbwa, paka au mbuzi, achilia mbali wababe kama Simba, Chui au Faru. Kiumbe huyo hatari wa kuogopwa kwa gharama yoyote ile ni MBU.
Kwa mujibu wa takwimu, Mbu ni kiumbe hatari zaidi kuliko wote duniani. Kiumbe huyo hatari ni maarufu kwa kuambukiza rundo la magonjwa, kubwa zaidi ikiwa ni homa ya malaria. Lakini pia mbu hueneza homa ya matende (elephantiasis), homa ya manjano (yellow fever), kindiga popo (dengue fever) na homa ya Mto Nile.
KESI DHIDI YAKE: Mbu anawajibika kusababisha kati ya vifo milioni 2 hadi 3 kwa mwaka.
VIJIWE (Hangout) VYAO: Takriban dunia nzima lakini zaidi barani Afrika, Asia na Amerika ya Kaskazini.
ANAVYOSABABISHA MAAFA: Mbu huambukiza maradhi ya kuuma kwenye ngozi ya binadamu na kumwaga mate yake yenye vijidudu vinavyosababisha homa husika. Ukiweka kando vipele vidogo vinavyotokea mahala alipouma mbu, anayeambukizwa na mbu hatambua maambukizo hadi pale kinga za mwili inaposhtuka (na kuleta dalili mbalimbali).
JINSI YA KUMKWEPA: Njia ya kupambana na mbu na maambukizo ni pamoja na kutumia chandarua kilichomwagiwa kinga, kuangamiza sehemu za mazalio ya mbu na vidonge vya kinga.
------------------------------------------------------------------------------------------
Nyoka Wenye Sumu Kali
Japo kuna zaidi ya aina 2,000 za nyoka, 450 kati yao wenye sumu,ni aina 250 tu kati yao ndio wenye uwezo wa kuua binadamu.
KESI DHIDI YAO: Nyoka wenye sumu kali husababisha kati ya vifo 50,000 na 250,000 kwa mwaka.
VIJIWE VYAO: Zaidi ni Afrika,Asia na Amerika ya Kaskazini
WANAVYOSABABISHA MAAFA: Nyoka wana kasi sana na sehemu yoyote katika mwili wa binadamu inaweza kuwa kugongwa na kiumbe huyo hatari.Lakini ni hatari zaidi nyoka anapomgonga mtu kwenye mshipa wa damu kwani hiyo huharakisha kusambaa kwa sumu ya kiumbe huyo.Nyoka hutumia sumu yao kumlegeza mtu na pengine kumpotezea fahamu.Majoka makubwa kama Mfalme Kobra (King Cobra) yanaweza kusimama hadi usawa wa kichwa cha binadamu,huku wengine wakiweza kutema na kurusha sumu yao kutoka mbali kwenda kwenye macho ya mwanadamu.
JINSI YA KUWAKWEPA: Mara nyingi nyingi nyoka hushambulia pale tu pale anapobughudhiwa.Kwahiyo ushauri muhimu wa kuepuka shambulizi kutoka kwa viumbe hao ni kujiepusha nao (Stay away!).Pia ni muhimu kuvaa mabuti kwenye mazingira yanayoweza kuwa na nyoka.Epuka mapori yanayoweza kuwa makazi ya nyoka.Na ikitokea umeomwona nyoka,inashauriwa urudi kinyumenyume taratibu kwani anaweza kujirusha mara nusu ya urefu wake,na mtikisiko kidogo tu unaweza kumasha hasira za kiumbe huyo hatari.
--------------------------------------------------------------------------------------------
Nge
Ni kiumbe hatari mwenye sura mbaya maradufu.Inaaminika kuwa ng'e anaweza kuwa anasababisha vifo vingi zaidi ya vile vinavyorekodiwa rasmi,sababu ya kuhisi hivyo ikiwa ni mazingira wanayoishi viumbe hao na ugumu wa kupatikana tiba dhidi ya sumu yao.Hata hivyo,japo kuna aina tofauti 1500 za ng'e ni 25 tu kati yao ambao ni hatari kwa uhai wa uhai wa binadamu.
KESI DHIDI YAO: Ng'e husababisha kati ya vifo 800 hadi 2,00 kwa mwaka
VIJIWE VYAO: Duniani kote hususan Afrika,America ya Kusini na Kaskazini na Asia ya Kati.
WANAVYOSABABISHA MAAFA: Ng'e humlegeza binadamu baada ya kumdunga sumu kwa kutumia "vijisindano" vilivyopo kwenye mikia yao.Kama ilivyo kwa sumu nyingine za wadudu/wanyama,binadamu walio hatarini zaidi ni wale wenye aleji,japo ng'e wengi wenye sumu wanaopatikana Afrika wanaweza kumdhuru mtu yeyote yule.
JINSI YA KUWAKWEPA: Ng'e huwa active zaidi nyakati za usiku na hupendelea kujipumzika mchana.Kwahiyo ni muhimu kuhakikisha sehemu ya kujilaza ipo salama kabla ya kuubwaga mwili.Kadhalika ni muhimu kupunga mavazi na/au soksi kuhakikisha hakuna ng'e humo,vinginevyo itakuwa balaa.
----------------------------------------------------------------------------------------------
WENGINEO KWA KIFUPI
Paka Wakubwa (Simba,Chui,nk)
Paka Wakubwa (kwa mfano yaani Simba,Chui,nk) husababisha takriban vifo 800 kwa mwaka
...............................................................................................
Mamba
Mamba husababisha kati ya vifo 600 na 800 kwa mwaka
............................................................................................
Tembo
Pamoja na upole wao,Tembo husababisha kati ya vifo 300 na 500 kwa mwaka
.............................................................................................
Kiboko
Mwamba huyo wa majini mwenye sura mbaya husababisha vifo kati ya 100 na 150 kwa mwaka
..............................................................................................
Konyeza (jellyfish
Kiumbe huyu wa baharini husababisha takriban vifo 100 kwa mwaka
..............................................................................................
Papa
Kiumbe huyu hatari wa baharini husababisha takriba vifo 100 kwa mwaka
...............................................................................................
Panda
Husababisha kati ya vifo 5-10 kwa mwaka
***********************************************************************************************
No comments:
Post a Comment