WELCOME ALL

Gonga Hapa.

Thursday, October 13, 2011

CHATU

Kiumbe huyu...Chatu(Python) ndo kati ya nyoka wachache duniani wenye meno zaidi ya 2 maana hawana sumu. Meno yao hutumika kukamata msosi mdoni na kuubana ili usikimbie. wanaua kwa kubana na kujizungusha kwa mnyama kumziba pumzi na kuvunja vunja mbavu na mifupa. Hapa alimeza Impala (Swala pala) . bahati mbaya akanasa kwenye fensi ya umeme..South border to Botswana...wadau wakamdaka akikata roho....Follow...
Hapa ameona fensi ndo nuksi akaamua king'ata kumbe ndo anapigwa shoti zaidi

Mnyama mwenewe aliyemeza anasazi kama hii hapa...alafu mtamu kuliko mbuzi,anaitwa mbawala kwa waliowahi tembelea mbuga za wanyama watakua wanamfahamu vizuri


Wadau walimchinja wakapata mboga mbili tofauti...nyama choma ya swala na mapande ya chatu ya kumwaga...Yummy!!



Huyu(sio chatu) alimeza yai kubwa la Mbuni (Ostrich). Hapo najiuliza je Nazi imeingiaje kwenye tumbo la nyoka!! viumbe hawa wamepewa uwezo wa kula vitu vikubwa sana kuliko hata maumbile yao lakini lazima waishi na lazima wale.


akameza yai linye ukubwa kama picha inavyoonyesha hapo chini

Simba Sports Club-Tanzania



Record: 8-2
Simba SC is a Tanzanian football club based in Dar es Salaam. Their home games are played at two stadiums Uhuru Stadium and National Stadium. Simba SC is one of two biggest football clubs in Tanzania, their archrivals being the Young Africans. The club had several names during its history, when it was founded in 1936 it was called Queens, then changed to Eagles, Dar Sunderland and later, in 1971 changed to its actual name, Simba (that means Lion in Swahili).

Simba is the biggest also the most titled club in Tanzania.
The highest level of success that Simba SC achieved was getting to the final of the CAF Cup in 1993 where they lost to Stella Abidjan of Ivory Coast. It was the highest achievement on continental competitions reached by any Tanzanian team. One of the most memorable years for the club was 2003 when it knocked off the then reigning champions Egyptian giants Zamalek on its way to qualify for the group stages of the CAF Champions League. In the first round of that year's competition, Simba SC eliminated Santos of South Africa.
African Cup of Champions Clubs: 8 appearances
1974: Semi-Final
1976: Second Round
1977: Second Round
1978: Second Round
1979: Second Round
1980: Second Round
1981: First Round
1995: Second Round

CAF Confederation Cup: 2 appearances
2007 - Preliminary Round
2010 -
CAF Cup: 2 appearances
1993 - Finalist
1997 - First Round
CAF Cup Winners' Cup: 3 appearances
1985 - Second Round
1996 - Second Round
2001 - Second Round


Tanzanian Premier League: 17
1965, 1966 (as Sunderland)
1972, 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1993, 1994, 1995, 2001, 2002, 2004, 2007, 2009/2010
Tanzanian Cup: 3
1984, 1995, 2000
Tanzanian Tusker Cup: 5
2001, 2002, 2003, 2005
2005 in Kenya
CAF Cup:
Finalist : 1993



CECAFA Clubs Cup: 6
1974, 1991, 1992, 1995, 1996, 2002
[edit] Performance in CAF competitions
CAF Champions League:
2002 - First Round
2003 - Group Stage
2004 - First Round
2005 - First Round
2008 - First Round
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen Pichani



amesema hapati shinikizo lolote kutokana na kauli ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mbrazili Marcio Maximo kwamba yuko tayari kurudi kufundisha Stars. Maximo alinukuliwa na gazeti hili akisema yupo tayari kurudi nchini kuifundisha Taifa Stars, kama Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakimhitaji kufanya hivyo.

Akizungumza Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana baada ya Stars kurejea ikitokea Morocco ilikofungwa mabao 3-1 Jumapili na kushindwa kufuzu fainali za Afrika mwakani, alisema hasumbuliwi na kauli hiyo kwani bado ana mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha Stars. “Sina presha na alichokisema kocha huyo, zaidi ya yote bado nina mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha timu hii na ninachoangalia ni kuiandaa timu kwa ajili ya michuano ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia,” alisema Poulsen. Maximo alikaririwa juzi pamoja na mambo mengine akikosoa utaratibu wa sasa wa kutoinua vijana na badala yake kuita katika timu ya Taifa wachezaji wakongwe kwa sababu tu wanaishi Ughaibuni. Pia alishangaa kusikia kuwa hivi sasa Mrisho Ngassa anakalishwa benchi katika timu ya Taifa na kuingia baadaye, wakati ni mchezaji mahiri na kusema kuwa kufanya hivyo ni kuua kiwango chake. Tayari Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema linasubiri ripoti ya kocha huyo ili kujua nini kifanyike kuboresha timu hiyo. Hata hivyo akizungumza jana kuhusu Stars kushindwa kufuzu fainali hizo, Poulsen alisema, wamefungwa na timu bora yenye wachezaji wengi wanaocheza Ulaya na Ligi Kuu ya England. Poulsen alisifu kiwango kilichooneshwa na timu yake kwa kudai kuwa wachezaji wake walionesha mchezo mzuri na kujituma muda wote. Akizungumzia mchezo ujao dhidi ya Chad kuwania kuingia makundi ya mchujo kwa ajili ya michezo ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2014, Poulsen alisema atabadilisha kidogo kikosi hicho na kwamba wachache kati ya wachezaji waliopo sasa ndio watakaokosekana. “Nitawezaje kubadili kikosi chote? Haiwezakani, wengi watakuwepo wachache watakosekana,” alisema Poulsen.

Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa

Wasanii maarufu wa Orijino Komedi na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ na bendi yake ya Machozi wanatarajiwa kutumika kutunisha mfuko utakaofanikisha Siku ya Utalii Duniani, ambayo kitaifa itafanyika mkoani hapa. Zaidi ya Sh milioni 120 zimekadiriwa kutumika kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe hiyo itakayofanyika kwa wiki nzima kuanzia Septemba 28 hadi Oktoba 4, mwaka huu.



Mratibu wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe hizo, Fidiah Nakamendu alisema jana kwenye kikao cha maandalizi kwamba sherehe hizo zitafanyika nje kidogo ya Manispaa ya Iringa katika Kijiji cha Nduli, karibu na Uwanja wa Ndege wa Nduli. Alisema wasanii hao watafanya maonyesho yao katika mabonanza yatakayoandaliwa baadaye mjini Iringa. Alitaja mikakati mingine itakayofanikisha upatikanaji wa fedha hizo kuwa ni pamoja na kutuma barua za maombi ya michango kwa wadau mbalimbali wa utalii kama asasi za kiserikali na zisizo za kiserikali.





Mikakati mingine ni pamoja na kuandaa chakula cha hisani na kufanya tamasha la kitamaduni la chakula, mavazi na ngoma za asili. Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Mrisho ambaye ni Mwenyekiti wa sherehe hizo, ameagiza kamati hiyo ifungue akaunti maalumu ya sherehe itakayokuwa na wajumbe wawili kutoka sekta ya umma na wengine wawili kutoka sekta binafsi na kuupongeza uamuzi wa kamati kufanyia sherehe hizo karibu na Uwanja wa Ndege wa Nduli kwani utaongeza changamoto katika kuendeleza utalii wa Mkoa wa Iringa. Kulingana na waandaaji, wakati wa sherehe hizo wageni watapata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo mkoani hapa kwa gharama nafuu, pia kutakuwa na maonyesho ya vikundi mbalimbali vya burudani.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Waziri Mkuu TUME YA KUDHIBITI UKIMWI TANZANIA

BOHARI Kuu ya Dawa nchini (MSD) imesema idadi kubwa ya dawa za kupunguza makali ya Ukimwi (ARVs) kwenye maghala yake zimekwisha muda wa matumizi na moja ya sababu ikiwa ni kuingizwa kwa dawa hizo na wafadhili bila kuzingatia mahitaji.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Joseph Mgaya aliieleza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi Dar es Salaam jana kuwa, Tanzania haina tatizo la dawa hizo za kurefusha maisha kwa sasa, ingawa nyingi zilizopo hazifai tena.

Akifafanua, Mgaya alisema tatizo hilo linatokea zaidi kwa ARVs za fungu la pili, zinazoletwa na wafadhili kutoka nje, maalumu kwa wagonjwa wa Ukimwi ambao virusi vinavyoshambulia kinga zao za mwili vimeshindwa kupozwa na dawa za fungu la kwanza.

“Dawa hizi tunazitegemea kutoka kwa wafadhili pekee kwa sababu Serikali haihusiki kuzinunua, zinaletwa kwetu kama msaada hasa na Mfuko wa Rais wa Marekani wa Kusaidia Mapambano dhidi ya Ukimwi (PEPRAR) kwa wagonjwa ambao virusi vinavyowashambulia ni sugu.

“Kwa kweli asilimia kubwa ya dawa hizi tulizonazo sasa zimeharibika na tumegundua sababu mbalimbali zinazochangia hali hiyo, kuwa ni pamoja na kuletwa kwa wingi bila kuzingatia mahitaji, kukosekana kwa kemikali za kupima mwendelezo wa CD4 (aina ya vitendanishi) kwa wagonjwa walioanza kutumia ARVs,” alisema Mgaya.

Sababu nyingine aliyoitaja ni kukosekana kwa fedha za kukomboa dawa hizo kutoka bandarini, mara zinapowasili kutoka nje, kutokana na utaratibu uliowekwa na Serikali unaohitaji hatua nyingi ili kupata fedha kwa ajili ya shughuli kama hiyo. Hali hiyo, alisema imesababisha dawa hizo zianze kupungua uhai wake kabla hata ya kuingia kwenye maghala hayo.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi wa MSD, Heri Mchunga aliiambia Kamati hiyo kuwa, pamoja na sababu hizo, kumekuwa na utaratibu usiofaa wa Serikali kubadili miongozo ya aina za dawa zinazofaa kutumika kwa wagonjwa hao, bila kuzingatia uwepo wa dawa za awali katika bohari hiyo.

Hata hivyo, Mfamasia Mkuu wa Serikali, Joseph Muhume alifafanua kwamba Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii haiwezi kubadilisha miongozo ya matumizi ya dawa ghafla, bila utaratibu na bila maelekezo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) na kwamba, wanaofanya hivyo ni wahusika katika vituo vya afya wenyewe.

“Ni kweli kuna tatizo la wagonjwa kubadilishiwa miongozo ya dawa kiholela. Wakati wanapaswa kutumia hizo za kundi la pili, unakuta wamehamia kwenye dawa nyingine na kuzifanya zilizopo kukosa watumiaji na kuharibika, huku hali halisi ya uhitaji ikiendelea kuwepo. Serikali inalifanyia kazi suala hili,” alisema Muhume.

Alisema Serikali inatekeleza wajibu wake wa kuhakikisha kuwa dawa zote zinazoingia nchini zina asilimia 80 ya uhai, ikiwa na maana kuwa, asilimia 20 pekee ya uhai huo ndio unayoruhusiwa kisheria kupotea njiani.

Wakati huo huo, MSD imekiri kuwepo kwa tatizo la vitendanishi vinavyosaidia kugundua endapo mpimwaji ana VVU au la, na kusema tatizo hilo limechangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa fedha za kuvinunulia huku utegemezi wa fedha kutoka kwa wafadhili ukiwakwamisha kutokana na kutozituma kwa wakati.

Mgaya alisema, mahitaji ni makubwa kuliko uwezo wao wa kununua vitendanishi hivyo kutokana na kupewa mgawo mdogo sana wa fedha kwa ajili ya ununuzi wa dawa nyingine.

“Kwa mfano katika mwaka wa fedha 2011/2012, tuliomba shilingi bilioni 158 kwa ajili ya kufanya ununuzi huo, lakini tukatengewa shilingi bilioni 78 tu. Changamoto hii ni kubwa sana katika kutekeleza mapambano dhidi ya Ukimwi na kinachokwaza zaidi ni utegemezi wetu kwa wafadhili katika kuuendeleza mradi wa Ukimwi,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa MSD.

Hata hivyo, Muhume alijibu kuwa Serikali haina budi kuendelea kuwategemea wafadhili hao kwa sababu ni masikini na kwamba inachokitenga ndio uwezo wake, licha ya kujua ukubwa wa tatizo.

Muhume aliieleza kamati hiyo kuwa baada ya kujulishwa tatizo hilo na MSD, Serikali ilifanya jitihada na kuingiza nchini vitendanishi 34,000 vitakavyotosha kuihudumia nchi kwa miezi minne pekee, huku ikisubiri kuletewa vingine kwa ajili ya kupima CD4, vinavyotarajiwa kufika nchini mwishoni mwa mwezi huu.

“Tunafanya tuwezalo kuhakikisha kuwa hadi mwisho wa Novemba tatizo la dawa za kupima VVU linakwisha kabisa,” alisema na kuelezwa na wabunge kuwa akiwa mwakilishi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anapaswa kuifikishia Serikali ujumbe wa kufanya uamuzi wa kujitegemea katika vita dhidi ya Ukimwi vinginevyo wananchi wataangamia.